• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

Serikali Yatoa Matrekta 33 kwa Wakulima Wilayani Magu

Posted on: March 21st, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mheshimiwa Dkt. Philemon Sengati (PhD), leo tarehe 20.03.2019 amekabidhi matrekta 13 kwa vyama vya msingi vya ushirika, yaliyotolewa na Serikali kwa njia ya mkopo kupitia Benki ya Maendelo ya kilimo (TADB). Matrekta hayo yalikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa.

DC Sengati amesema kuwa Wilaya ya Magu inatarajia kupatiwa jumla ya matrekta 33 ambayo yanatolewa kwa awamu tatu, 13 tayari yamekabidhiwa, 12 yatakuja awamu ya pili na 8 yatatolewa awamu ya tatu. Pia amempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uzalendo wake dhamira na ndoto yake ya kulipeleka Taifa katika uchumi wa kati wa Viwanda. “Hivyo ili viwanda vifikiwe lazima tuwekeze katika kilimo ambacho ndicho huzalisha mali ghafi kwa ajili ya viwanda. Matrekta yataenda kufanya mapinduzi makubwa katika Kilimo na tutalima kwa tija na kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara”.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Lutengano George Mwalwiba ameipongeza Serikali kwa kutoa matrekta kwa Wakulima kitendo ambacho kitachochea ukuaji wa uchumi kwa Wanamagu, na kuwaondoa wananchi katika kilimo duni cha jembe la mkono vilevile ameshukuru watendaji wa Idara ya kilimo, umwagiliaji na ushirika kwa kuhamasisha uanzishwaji wa vyama vya ushirika ambapo kwa mwaka jana vilifanya vizuri kwa mkoa wa Mwanza pia kwa kuratibu vizuri mchakato wa upatikanaji wa matrekta hayo.

Vyama vya ushirika vilivyopewa kwa awamu ya kwanza ni Igunabalimi (Jinjimili), Masengese (Kabale), Nhobola, Ndagalu, Chandulu, Mahaha, Shishani, Nsobu (Nsola Bubinza) Mwalinha, Lugeye, Nyanguge, na Bugatu. DC Sengati amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kusimamia vizuri vyombo hivyo kwa mujibu wa taratibu na kwamba viziwe chanzo cha migogoro na vikatumike kwa maslahi mapana ya jamii na wanachama wa vyama hivyo. Pia amewaasa kufuata vigezo walivyopewa ikiwemo kufanya marejesho kwani mkopo huo umetolewa kwa asilimia mia moja kwa udhamini wa Serikali.

Nao viongozi wa vyama vya ushirika wameipongeza Serikali kwa utendaji kazi wake uliotukuka, “kwa Kweli Matrekta haya yanaenda kuamsha ari ya wakulima kupanua zaidi shughuli zetu za kilimo na kusaidia kuondakana na umasikini  na Tunawaahidi kuwa tutafanya kazi kwa uaminifu kama Serikali ilivyotuamini” Amesema Mwenyekiti wa AMCOS Mahaha.

Magu Kazi na Maendeleo- Kusema na kutenda

Matangazo

  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari mwaka 2020 Magu DC December 12, 2019
  • Usajili wa kidato cha nne na cha pili kwa ngazi ya wilaya February 17, 2017
  • Mazoezi ya Viungo kwa wafanyakazi na wananchi February 08, 2017
  • Usafi wa Mazingira. February 16, 2017
  • Angalia zote

Habari mpya

  • Hatua mbalimbali za ujenzi wa miradi ya Maendeleo magu

    November 01, 2019
  • Naibu Waziri Awataka Waajiri Kutenga Muda wa Kusikiliza Kero za Watumishi Katika Maeneo yao ya Kazi

    October 04, 2019
  • DC Magu azindua Kampeni ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto

    September 30, 2019
  • Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka, 2019

    September 23, 2019
  • Angalia zote

Video

Fahamu Maendeleo ya Wilaya ya Magu Ndani ya Serikali ya Awamu ya Tano
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa